×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Kuwepo kwa Mungu

Je kuna Mungu?

Je, Mungu yupo? Hapa kuna sababu sita za moja kwa moja za kuamini kwamba kweli Mungu yuko.

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Mara moja tu, Je, si ungependa mtu akuonyeshe tu ushahidi wa kwamba Mungu yupo? Hakuna kupotosha. Hakuna kauli za, "Lazima tu uamini." Naam, na hapa kuna baadhi ya sababu zinazojaribu kuonesha kwa uwazi kwamba Mungu yupo.

Lakini kwanza fikiria hili. Inapohusu uwezekano wa kuwepo kwa Mungu, Biblia inasema kwamba kuna watu ambao wameona uthibitisho wa kutosha, lakini wameficha ukweli juu ya Mungu.1 Kwa upande mwingine, kwa wale wanaotaka kumjua Mungu kama yeye yuko, anasema, “Mtanitafuta na kuniona; mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote, nami nitaonekana kwenu.”2

Kabla ya kutazama uhakika wa mambo yanayohusu uwepo wake, jiulize, Ikiwa Mungu yupo, je, ningependa kumjua? Hapa basi, kuna baadhi ya sababu za kuzingatia…

1. Utata wa sayari yetu unaelekeza kuwa kuna Mbunifu ambaye sio tu aliumba ulimwengu wetu, bali pia anauhusimamia hata leo.

Kuna mifano mingi inayoonesha Mungu aliiumba, yamkini bila mwisho, na hapa tumeweka mifano michache:

Dunia...ukubwa wake ni kamilifu. Saizi ya Dunia na uvutano wake hushikilia safu nyembamba ya gesi nyingi za nitrojeni na oksijeni, inayoenea tu kama maili 50 juu ya uso wa Dunia. Ikiwa Dunia ingekuwa ndogo, angahewa isingewezekana, kama sayari ya Mercury. Ikiwa Dunia ingekuwa kubwa zaidi, angahewa yake ingekuwa na hidrojeni ya bure, kama Jupiter.3 Dunia ndiyo sayari pekee inayojulikana kuwa ina angahewa ya mchanganyiko sawa wa gesi ili kuendeleza maisha ya mimea, wanyama na wanadamu.

Picha inayoonyesha ukubwa wa kadiri wa dunia na umbali kamili kwa jua kama uthibitisho wa kuwako kwa Mungu katika kuumba ulimwengu.Dunia iko kulia umbali kutoka kwa Jua. Picha ya kawaida ya mlango wa mbele wa nyumba. Ikiwa Jua lingekuwa juu ya fremu ya mlango, Dunia ingekuwa kama sarafu ndogo iliyoketi kwenye fremu ya chini ya mlango.4

Fikiria mabadiliko ya joto tunayokutana nayo, takriban digrii -30 hadi digrii +120. Ikiwa Dunia ingekuwa mbali zaidi na jua, sote tungeganda. Karibu na tungeungua. Hata utofauti wa sehemu katika nafasi ya Dunia kwa jua ungefanya maisha duniani yasiwezekane.

Dunia inabaki imara katika umbali wake kutoka kwenye jua uku ikilizunguka jua karibu na kasi ya 67,000mph. Pia ikijizungusha katika mwimili wake. Ikiruhusu uso mzima wa Dunia kupata joto na kupozwa kila siku vizuri.

Na Mwezi wetu una saizi kamili na umbali wa kutoka katika Dunia kwa uvutano wake. Mwezi huunda mawimbi muhimu na muzunguko kufanya maji ya bahari yasimwagike, na bado bahari zetu zimezuiwa zisimwage maji yake katika mabara yote.5

Maji...hayana rangi, hayana harufu na hayana ladha na bado hakuna kiumbe hai kinaweza kuishi bila hayo. Mimea, wanyama na binadamu hujumuishwa maji zaidi (karibu theluthi mbili ya mwili wa binadamu ni maji). Utaona kwanini sifa za maji zinafaa kwa maisha.

Yana ukingo mpana kati ya kiwango cha kuchemka na kiwango cha kuganda. Maji huturuhusu kuishi mazingira yenye mabadiliko ya joto, ambapo uweka miili yetu sawa na digrii 98.6.

Picha kutoka chini ya maji katika ziwa au bahari ili kuonyesha zaidi ya maji ambayo Mungu aliyabuni, kwamba maji huganda kutoka juu kwenda chini, ili kuruhusu samaki kuishi wakati wa baridi.Maji ni kiyeyusho cha ulimwengu wote kinachoruhusu kemikali, madini na virutubisho kwa urahisi kuyeyuka na kubebwa katika miili yetu kwenye mishipa midogo zaidi ya damu.6

Maji pia hayana kemikali. Bila kuathiri muundo wa chembechembe yanayobeba, maji usaidia chakula, dawa na madini kufyonzwa na kutumiwa na mwili.

Maji yana mvuto wa kipekee. Maji katika mimea yanaweza kutililika juu kinyume cha uvutano, kuleta uhai na virutubisho juu hata kama miti ni mirefu sana.

Maji huganda kutoka juu kwenda chini na kuelea, hivyo samaki wanaweza kuishi wakati wa baridi.

Picha ya mvua inayonyesha kwenye mimea, inayoonyesha mchakato wa uvukizi na usambazaji wa maji kwenye sayari yetu muhimu kwa uhai, uthibitisho mwingine wa kwamba Mungu yuko.Asilimia tisini na saba ya maji ya Dunia yako baharini. Lakini Duniani, kuna mifumo ya kuondoa chumvi kutoka hayo maji na kuyasambaza maji hayo duniani kote. Uvukizi huchukua maji ya bahari, na kuacha chumvi na kutengeneza mawingu ambayo ni rahisi kuamishwa na upepo ili kuyatawanya juu ya mimea iliyo katika nchi, kwa wanyama na kwa watu. Ni mfumo wa uchenjuaji na kuendeleza usambaza maisha katika sayari hii, ni mfumo wa uchakataji na kuyatumia tena hayo maji.7

Ubongo wa mwanadamu...huchakata habari haraka kiasi cha kushangaza. Ubongo wako uchukua rangi zote na vitu unavyoviona, halijoto inayokuzunguka, mgandamizo kati ya miguu yako na sakafu, sauti zinazokuzunguka, ukavu wa kinywa chako, umbile la simu yako ya mkononi. Ubongo wako ubeba na uchakata hisia zako, mawazo na kumbukumbu zako zote. Wakati huo huo ubongo wako unafuatilia kazi zinazo endelea katika mwili wako kama kupumua, mwendo wa kope, njaa na mjongea wa misuli za mikono yako.

Picha ya mwanamke akiwaza, ili kuonyesha uwezo wa ubongo wa mwanadamu wa kuchakata jumbe milioni moja kwa sekunde, uwezo wa ajabu unaojibu swali, 'Je kuna Mungu?'Ubongo wa mwanadamu huchakata zaidi ya jumbe milioni moja kwa sekunde.8 Ubongo wako ubeba taarifa muhimu, na kuchuja zisizo muhimu. Kazi ya kuchuja ni ile inayokuruhusu wewe uzingatie na ufanye kazi kwa ufanisi katika ulimwengu wako. Kazi za ubongo wako ni tofauti na za viungo vingine. Kuna hekima katika hilo, uwezo wa kufikiri, kuzalisha hisia, kuota na kupanga, kuchukua hatua na kuhusiana na watu wengine.

Jicho...linaweza kutofautisha kati ya rangi milioni saba. Lina lenga lenyewe na kushughulikia jumbe milioni moja na nusu (1.5) kwa pamoja.9 Mageuzi uzingatia mabadiliko na mabadiliko kutoka na ndani ya viumbe vilivyopo. Bado mageuzi peke yake hayana uwezo wa kueleza chanzo cha jicho au ubongo…. Chanzo cha kuanza kwa viumbe hai kutoka kwenye maada zisizo hai.

2. Je, Mungu ni kweli? Ulimwengu ulikuwa na mwanzo – ni kilisababisha?

Wanasayansi wanaamini kuwa ulimwengu ulianza na mlipuko mmoja wa nguvu na mwanga, ambao sasa tunauita BIG BANG. Huo ulikuwa ni umoja ulioanza kwa kila kitu kuwepo: kuanza kwa ulimwengu, kuanza kwa nafasi na pia kuanza kwa mda wenyewe.

Picha inaonyesha mlipuko wa nuru ili kuonyesha mwanzo wa ulimwengu, sambamba na Mungu aliposema, 'Iwe nuru.'Mwanafizikia wa nyota Robert Jastrow, aliyejieleza kwa mashaka, na kusema. “Mbegu ya kila kitu ambacho kimetukia Ulimwenguni kilipandwa katika muda huo wa kwanza; kila nyota, kila sayari na kila kiumbe hai katika Ulimwengu kilikuja kuwa tokeo la matukio ambayo yalianza wakati wa mlipuko wa ulimwengu ... Ulimwengu uliangaza na kuwa, na hatuwezi kujua ni nini kilisababisha hilo kutokea."10

Steven Weinberg, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia, alisema wakati wa mlipuko huu, "ulimwengu ulikuwa wa digrii za Sentigredi laki elfu...na ulimwengu ulijaa nuru."11

Ulimwengu haujakuwepo sikuzote. ulikuwa na mwanzo ... nini kilisababisha hilo? Wanasayansi hawana maelezo ya mlipuko wa ghafla wa mwanga na maada.

3. Ushahidi kwa Mungu: Ulimwengu unafanya kazi kwa sheria zinazofanana za asili. Kwa nini hivyo?

Sehemu kubwa ya maisha inaweza kuonekana kutokuwa sawa, lakini angalia kile tunachoweza kuhesabu siku baada ya siku: nguvu ya uvutano inabaki thabiti, kikombe cha kahawa cha moto kinachoachwa kwenye kaunta kitapoa, dunia inajizungusha kwa saa 24, na kasi ya mwanga haitabadiliki -- duniani au kwenye galaksi zilizo mbali kutoka kwetu.

Sayansi zote--biolojia ya molekuli, kemia, fizikia, unajimu, n.k.--zinategemea sheria thabiti za asili.

Dk. Emily Baldwin alitoa maoni, "Moja ya namba muhimu zaidi katika fizikia, uwiano wa molekuli ya protoni-elektroni, ni sawa katika galaksi ya umbali wa miaka bilioni sita ya mwanga kama ilivyo hapa Duniani..."12

Picha ya milinganyo ya hesabu kama zinavyoonekana ubaoni ili kuonyesha asili ya hesabu ya sheria zetu za asili, ni uthibitisho mwingine kwamba Mungu yuko.Je! ni jinsi gani tunaweza kutambua sheria za asili ambazo kamwe hazitabadilika? Kwa nini ulimwengu ni wenye utaratibu na wenye kutegemeka sana?

"Wanasayansi wakuu wameshangazwa na jinsi jambo hili lilivyo la ajabu. Hakuna ulazima wa kimantiki kwamba ulimwengu unatii sheria, achilia mbali ule unaofuata kanuni za hisabati. Mshangao huu unatokana na utambuzi kwamba ulimwengu haulazimiki. Ni rahisi kufikiria ulimwengu ambao hali hubadilika bila kutabirika kutoka papo hapo hadi papo hapo, au hata ulimwengu ambamo vitu hutoka na kutoka."13

Mwanafizikia Paul C. Davies, anatoa maoni, “…ili uwe mwanasayansi, ulipaswa kuwa na imani kwamba ulimwengu unatawaliwa na sheria zinazoaminiwa, zisizobadilika, kamili, za ulimwengu mzima, za hisabati…”14

Uwezo wetu wote wa kugundua, kutatua matatizo, kuumba kumewezesha sheria zenye utaratibu za ulimwengu ambazo azibadiliki na zinaweza kupimwa kwa usahihi.

Richard Feynman, mshindi wa Tuzo ya Nobel ya quantum electrodynamics, alisema, "Kwa nini asili ni hisabati yenye fumbo...Ukweli kwamba kuna kanuni kabisa ni aina ya muujiza."15

4. Mtayarishaji wa Kiungu: Namba za DNA zinaarifu, zinapanga tabia ya seli

Picha inaonyesha ukuta wenye mpangilio wa sifuri ili kuonyesha kwamba molekuli bilioni 3 za DNA ambazo Mungu aliumba katika kila seli ya mwanadamu ni kama programu ya kompyuta.Maelekezo yote, mafundisho yote, mafunzo yote huja kwa nia. Mtu anayeandika mwongozo wa maagizo hufanya hivyo kwa kusudi. Je, unajua kwamba katika kila seli ya miili yetu kuna maelezo mengi ya kina, kama vile programu ndogo ya kompyuta?

Kama unavyojua, programu ya kompyuta imeundwa na moja na sufuri, kama hii: 110010101011000. Njia ambayo imepangwa ni ili iambie programu ya kompyuta nini cha kufanya. Namba ya DNA katika kila seli zetu zinafanana sana. Imeundwa na vitengo vinne vya kemikali, vinavyoitwa besi za nyukleotidi, ambazo wanasayansi hufupisha kama A, T, G, na C. Hizi zimepangwa katika seli ya binadamu kama hii: CGTGTGACTCGCTCCTGAT na kadhalika. Kuna jozi bilioni tatu za herufi hizi katika kila seli ya mwanadamu.15b

Vema, kama vile unavyoweza kupanga simu yako isikike kwa sababu maalum, DNA huelekeza seli. DNA ni mpango changamano, uliopangwa kuiambia seli kutenda kwa njia fulani. Ni mwongozo kamili wa maagizo.16

Uthibitisho wa Mungu upo - Picha ya herufi za karibu za DNA na CGTA zenye kitanzi cha kukuza, ili kuonyesha kemikali bilioni 3 za DNA zilizopangwa ndani ya kila seli ya binadamu.Kwa nini hii ni ajabu sana? Inabidi mtu aulize....programu hii ya habari iliishia vipi katika kila seli ya mwanadamu? Hizi sio kemikali tu. Hizi ni kemikali zinazofundisha, kanuni hiyo kwa njia ya kina sana jinsi mwili wa mtu unapaswa kufanya kazi.

Ni asili, sababu za kibaolojia zilizokosa maelezo lini taarifa hizo ziliundwa. Uwezi kupata maagizo, taarifa sahihi kama hii, bila kumpata mtu mwenye kuijenga kwa makusudi.

5. Tunajua Mungu yupo kwa sababu anatufuatilia. Yeye daima anaanzisha na kututafuta sisi twende kwake.

Wakati mmoja nilikuwa mtu asiyeamini kuwa kuna Mungu. Na kama watu wengi wasioamini kwamba kuna Mungu, suala la watu kumwamini Mungu lilinisumbua sana. Je, ni nini kuhusu wasioamini kwamba tungetumia muda mwingi, kwa umakini, na nguvu nyingi kukanusha jambo ambalo hatuamini hata lipo?! Ni nini kinachotufanya tufanye hivyo?

Nilipokuwa mtu asiyeamini kwamba kuna Mungu, nilihusisha nia yangu kama kuwajali wale maskini, watu wanaoishi mazingira magumu...kuwasaidia kutambua kwamba tumaini lao halikuwa na msingi wowote. Kusema kweli, nilikuwa pia na nia nyingine. Nilipokuwa nikiwapa changamoto wale waliomwamini Mungu, nilitamani sana kuona kama wangeweza kuniaminisha vinginevyo. Sehemu ya hamu yangu ilikuwa kuwa huru kutokana na swali la Mungu. Ikiwa ningeweza kuthibitisha kwa hakika kwa waumini kwamba walikosea, basi suala hilo haliko mezani, na ningekuwa huru kuendelea na maisha yangu.

Picha ya machweo ya jua kwenye ufupi wa bahari ili kuonyesha joto la upendo wa Mungu kwetu.Sikutambua kwamba sababu ya mada ya Mungu kunielemea sana akilini mwangu, ilikuwa ni kwa sababu Mungu alikuwa anasisitiza suala hilo. Nimekuja kugundua kwamba Mungu anataka kujulikana. Alituumba kwa nia ya kwamba tumjue. Ametuzunguka kwa ushahidi wake mwenyewe na analiweka swali la kuwepo kwake mbele yetu moja kwa moja.

Ilikuwa ni kana kwamba singeweza kuepuka kufikiria uwezekano wa Mungu. Kwa hakika, siku nilipochagua kukiri kuwepo kwa Mungu, maombi yangu yalianza kwa kusema, “Sawa, umeshinda...” Huenda ikawa sababu ya msingi ya watu wasioamini kuwa hakuna Mungu wanasumbuliwa na watu wanaomwamini Mungu ni kwa sababu Mungu anawafuatilia kwa bidii.

Sio mimi pekee niliyepitia haya. Malcolm Muggeridge, mwandishi wa kisoshalisti na falsafa, aliandika, "Nilikuwa na dhana kwamba kwa namna fulani, mbali na kuuliza, nilikuwa nikifuatiliwa." CS Lewis alisema alikumbuka, "...usiku baada ya usiku, nikihisi kila akili yangu ilipoinuka hata kwa sekunde moja kutoka kwa kazi yangu, ukaribu thabiti, usio na kikomo wa Yeye ambaye nilitamani sana kukutana naye. Nilikubali, na nikakubali kwamba Mungu alikuwa Mungu, na akapiga magoti na kuomba: labda, usiku huo, mtu aliekataliwa na kukata tamaa ameokoka katika Uingereza.”

Lewis aliendelea kuandika kitabu kiitwacho, "Surprised by Joy" ni matokeo ya kumjua Mungu. Mimi pia sikuwa na matarajio yoyote zaidi ya kukiri kwa haki kuwako kwa Mungu. Hata hivyo katika miezi kadhaa iliyofuata, nilishangazwa na upendo wake kwangu.

6. Tofauti na ufunuo mwingine wowote wa Mungu, Yesu Kristo ndiye uthibitisho wa wazi zaidi, wa wazi kabisa wa Mungu kujifunua kwetu.

Kwa nini Yesu? Tazama katika dini zote kuu za ulimwengu na utapata kwamba Buddha, Muhammad, Confucius na Musa wote walijitambulisha kama walimu au manabii. Hakuna hata mmoja wao aliyewahi kudai kuwa sawa na Mungu. Kwa kushangaza, Yesu alifanya hivyo. Hilo ndilo linalomtofautisha Yesu na wengine wote. Alisema Mungu yupo na wewe unamwangalia.

Ingawa alizungumza juu ya Baba yake wa mbinguni, haikuwa sehemu ya matengano, bali ya muungano wa karibu sana, wa pekee kwa wanadamu wote. Yesu alisema kwamba yeyote aliyemwona yeye amemwona Baba, yeyote aliyemwamini, alimwamini Baba.

Picha ya mtu kusoma Biblia ili kuonyesha kwamba Mungu amefunua kwamba yeye yupo kwetu katika Bible.Basi Yesu akawaambia tena akasema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”17 alidai sifa na Utukufu ni za Mungu pekee: kuwa na uwezo wa kusamehe watu wa dhambi yao, huru kutoka tabia ya dhambi, kuwapa maisha mzuri na kuwapa uzima wa milele mbinguni.

Tofauti na walimu wengine ambao ulilenga watu kwa maneno yao, Yesu alichagua watu wake. Yeye hakusema, "kufuata maneno yangu na utapata ukweli." Yesu akamwambia, “Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.”18

Nini ushahidi Yesu alitoa kwa ajili ya kudai kuwa yeye ni Mungu?

Alifanya kile watu hawawezi kufanya. Yesu alifanya miujiza. Aliwaponya ... vipofu, vilema viziwi, hata waliwafufua wafu wengi. Alikuwa na mamlaka juu ya vitu ... aliumba chakula nje ya hewa nyembamba, cha kutosha kulisha umati wa watu elfu kadhaa.

Alifanya miujiza juu ya asili… kutembea juu ya ziwa, alikemea dhoruba lililokuwa linazunguka juu kwa baadhi ya marafiki inyamaze. Watu kila mahali walimfuata Yesu kwa kuwa mara kwa mara alikutana mahitaji yao, akifanya miujiza. Alisema mnisadiki ya kwamba mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu; la! Hamsadiki hivyo, sadikini kwa sababu ya kazi zenyewe.19

Yesu Kristo alionyesha Mungu kuwa ni mpole, mwenye upendo, na anafahamu kuwa tu wabinafsi na wenye mapungufu, lakini kwa undani anataka kuhusiana na sisi. Yesu ulionyesha kwamba ingawa anaona sisi kama wenye dhambi, kwa kuelewa kuwa tunastahili adhabu yake, upendo wake kwetu ulitawala na akaja na mpango tofauti.

Mungu mwenyewe alichukua umbo la mwanadamu na akakubali adhabu kwa ajili ya dhambi zetu kwa niaba yetu. Inasikika vibaya? Pengine, lakini baba wengi wenye upendo wangependelea maeneo ya biashara na watoto wao ndani ya wodi ya saratani kama wangeweza. Biblia inasema kwa sababu tunampenda Mungu ni kwa sababu alitupenda kwanza.

Yesu alikufa kwa ajili yetu ili tuweze kusamehewa. Katika dini zote zinazojulikana kwa wanadamu, ni kupitia Yesu pekee utamuona Mungu akiwafikia wanadamu, akitoa njia ya sisi kusiana nay eye. Yesu uthibitisha moyo wa Mungu wa upendo, ukutana na mahitaji yetu, utuvuta kwake.

Kwa sababu ya Yesu’ alikufa na kufufuliwa, yeye ametupa maisha mpya leo. Tunaweza kusamehewa, kukubaliwa kikamilifu na Mungu na kupendwa na Mungu kwa dhati. Akisema, “Naam nimekupenda kwa upendo wa milele, ndiyo maana nimekuvuta kwa fadhili zangu.”20 Huyu ni Mungu, katika matendo.

Kweli Mungu yuko? Kama unataka kujua, mchunguze Yesu Kristo. Tumeelezwa kuwa “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”21

Mungu hatulazimishi kumuamini, ingawa anaweza. Badala yake, ametoa ushaidi wa kutosha wa uwepo wake kwetu ili kwa hiari yetu tumuamini. Urefu kamili wa Dunia kutoka kwenye jua, upekee wa maji, Ubongo wa mwanadamu, DNA, idadi ya watu wanaoshudia kumjua Mungu, shauku inayokuwa mioyoni mwetu na akilini mwetu ya kutaka kujua kama Mungu yupo, mapenzi ya Mungu ya kutaka kujulikana kupitia kwa Yesu Kristo. Kama ungependa kumujua zaidi Yesu na sababu ya kumuamini yeye, tafadhali angalia: Kwanini Yesu ni Mungu.

Ushaidi Binafsi kwa Mungu: Kama unataka kuanza uhusiano na Mungu sasa, unaweza.

Hii ni uamuzi wako, hakuna kutumia nguvu hapa. Lakini kama unataka kusamehewa na Mungu na kuwa na uhusiano naye, unaweza kufanya hivyo sasa hivi kwa kumuomba akusamehe na umuombe na aje katika maisha yako. Yesu alisema, “Tazama, nasimama mlangoni [moyoni mwako], nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.”22

Kama unataka kufanya hivyo, lakini hauna uhakika jinsi ya kuiweka katika maneno, hii inaweza kusaidia: "Yesu, asante kwa kufa kwa ajili ya dhambi zangu. Unajua maisha yangu na kwamba ninaitaji msamaha. Ninakuomba unisamehe sasa na uje katika maisha yangu. Ninaitaji kukujua kwa namna ya kweli. Njoo katika maisha yangu leo. Asante kwamba ulitaka uhusiano na mimi. Amina.”

Mungu anaona uhusiano wako na yeye ni wa kudumu. Ukiwaangalia wale wote waliomuamini. Yesu Kristo alitwambia, “…nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.”23

Kuangalia mambo haya yote, mtu anaweza kuhitimisha kwamba Mungu mwenye upendo yupo na anaweza akajulikana kwa karibu sana, njia binafsi.

 Nilimpokea Yesu maishani mwangu (ujumbe muhimu unafuata)…
 Ninaweza kutaka kumuuliza Yesu maishani mwangu, tafadhali eleza hili kikamilifu zaidi…
 Nina swali…

[na Dkt. Marilyn Adamson]

Maelezo ya chini: (1) Warumi 1:19-21 (2) Yeremia 29:13-14 (3) R.E.D. Clark, Creation (London: Tyndale Press, 1946), p. 20 (4) https://solarsystem.nasa.gov/solar- system/sun/overview/ (5) The Wonders of God's Creation, Moody Institute of Science (Chicago, IL) (6) Ibid. (7) Ibid. (8) Ibid. (9) Hugh Davson, Physiology of the Eye, 5th ed (New York: McGraw Hill, 1991) (10) Robert Jastrow; "Message from Professor Robert Jastrow"; LeaderU.com; 2002. (11) Steven Weinberg; The First Three Minutes: A Modern View of the Origin of the Universe; (Basic Books,1988); p 5. (12) Dr. Emily Baldwin; "Earth's Laws Still Apply in Distant Universe"; AstronomyNow.com; June, 2008. (13) Dinesh D'Souza, What's So Great about Christianity; (Regnery Publishing, Inc, 2007, chapter 11). (14) Paul C. Davies, physicist, cosmologist, astrobiologist, at Arizona State University; quoted in edge.org/3rd_culture/davies07/davies07_index.html. (15) Richard Feynman, The Meaning of It All: Thoughts of a Citizen-Scientist (New York: BasicBooks, 1998), 43. (15b) https://www.genome.gov/human-genome-project/Completion-FAQ (16) Francis S. Collins, director of the Human Genome Project, and author of The Language of God, (Free Press, New York, NY), 2006 (17) Yohana 8:12 (18) Yohana 14:6 (19) Yohana 14:11 (20) Yeremia 31:3 (21) Yohana 3:16 (22) Ufunuo 3:20 (23) Yohana 10:27-29.


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More