Sikiliza makala hii:
Fikiria nyundo. Imeundwa kupiga misumari. Hivyo ndiyo ilivyouundwa kufanya. Sasa fikiria kwamba nyundo haitatumika. Ikaa tu kwenye kisanduku cha zana za kazi. Nyundo hiyo hatojali.
Lakini sasa fikiria nyundo hiyo pamoja na nafsi, katika kujitambua. Siku na Siku nafsi hiyo uenda na mtu kama kukaa kwenye kisanduku cha zana za kazi. Nafsi hiyo itajihisi furaha, lakini haijui kwa nini. Kuna kitu kinakosa, lakini haijui ni nini hasa kinakosa.
Siku moja mtu aichukue kutoka kwenye hicho kisanduku cha zana za kazi kisha atumie kuvunja matawi yaliyozunguka mti. Nyundo hiyo itafurahia. Ilivyoshikwa, ilivyobebwa, ilivyopiga matawi, nyundo imependezwa. Mwisho wa siku, hata hivyo itakuwa bado haijatimiza lengo. Kupiga matawi ilikuwa furaha, lakini haikutosha. Kuna jambo ambalo bado linakosa.
Katika siku zifuatazo, atakavyo itumia mara nyingi. Kwa kutengeneza tena kifuniko, kwa kupasua mwamba, kwa kugonga kurudishia mguu wa meza uliovunjika. Bado, kusudi halijitimizwa. Kwa hiyo inatamani hatua zaidi. Hivyo nyundo hiyo inataka kutumika zaidi iwezekanavyo kwa kugonga vitu vinavyoizunguka, kuvunja vitu, kupasua vitu na kungoa vitu. Inajihesabu kwamba haijapata kazi za kutosha ya kuridhisha. Zaidi ya hayo, inaamini, suluhisho ni kukosa kutumika.
Kisha siku moja mtu mmoja aliitumia kugonga msumari. Ghafla, mwanga ukatoka kwenye nafsi ya nyundo. Ikatambua ukweli wa kile ilichoundwa kufanya. Inamaanisha kupiga misumari. Mambo mengine ya kugonga ni ya kuoanisha. Sasa nyundo inajua nafsini mwake kile ilichokuwa inakitafta kwa muda mrefu.
Tumeumbwa kwa mfano wa Mungu ili tuwe na uhusiano naye. Kuwa katika uhusiano huo ndicho kitu pekee ambacho hatimaye kitatosheleza nafsi zetu. Mpaka tunamjua Mungu, tumepitia katika mambo mengi yenye kushangaza, lakini hatujagonga msumari. Tumetumiwa kwa madhumuni mazuri, lakini sio yale tulioumbiwa kuyafanya, hakuna hata moja tuliopitia lililotupa kuridhika. Augustino alifupisha kwa njia hii: “Wewe [Mungu] umetuumba kwa ajili yako na mioyo yetu haijatulia mpaka ipate raha yake Kwako.”
Uhusiano na Mungu ndicho kitu pekee kitakachozima shauku ya nafsi zetu. Yesu Kristo alisema, "Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu hataona njaa kamwe, na yeye aniaminiye hataona kiu kamwe." Tunakuwa njaa na kiu katika maisha yetu yote. Tunajaribu "kula" na "kunywa" kila aina ya vitu ili kutosheleza njaa na kiu yetu, lakini bado njaa na kiu vinabaki pale pale. Nimpaka tumjue Mungu.
Sisi ni kama nyundo. Sisi ni kama nyundo. Hatutambui ni nini kitakachomaliza ombwe, kwa kukosa kutimiliza kusudi katika maisha yetu. Hata katikati ya gereza la Nazi, Corri Ten Boom alimpata Mungu kuwa ni mwenye kuridhisha kabisa: “Msingi wa furaha yetu tungelijua wenyewe kuwa tumefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Tungeweza kuwa na imani katika Upendo wa Mungu…Mwamba wetu ambaye ana Nguvu kuliko giza totoro.”
Kwa kawaida tunapomweka Mungu nje, tunajaribu kupata kutimiliza kusudi katika kitu kingine nje ya Mungu. Tunaendelea “kula” au “kunywa” zaidi na zaidi, tukifikiri kimakosa kwamba ‘zaidi’ ni jibu la matatizo, lakini bado hatujawahi kutosheka.
Tamaa yetu kuu ni kumjua Mungu, kuwa na uhusiano na Mungu. Kwa nini? Kwa sababu ndivyo tulivyoumbwa. Je, umegonga msumari bado?
► | Jinsi ya kuanza uhusiano na Mungu |
► | Nina swali… |