×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Maisha yangu

Je, Mungu Hujibu Sala Zetu?

Je, unatafakari namna ya kuomba? Mungu anatuambia yeye atajibu maombi…

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Je, umewahi kumfahamu mtu ambaye kweli anamtumainia Mungu? Nilipokuwa mtu asiyeamini kwamba kuna Mungu, nilikuwa na rafiki mzuri ambaye alisali mara nyingi. Binti huyo angeniambia kila wiki juu ya jambo fulani alilokuwa akiamini kwamba Mungu atalisimamia. Na kila wiki niliona Mungu akifanya jambo hilo lisilo la kawaida kujibu maombi yake. Je, unajua ilivyovigumu kwa mtu asiye muamini Mungu kukaa kusubiri Mungu ajibu maombi wiki baada ya wiki? Baada ya muda, “bahati mbaya” huanza kusikika kama hoja dhaifu sana.

Sasa kwa nini Mungu alijibu maombi ya rafiki yangu? Sababu kubwa ni kwamba alikuwa na uhusiano na Mungu. Alitaka kumfuata Mungu. Na kwa kweli alisikiliza kile alichosema. Akilini mwake, Mungu alikuwa na haki ya kumwelekeza katika maisha yake, naye umkaribisha kwa kufanya tu hivyo! Anaposali kwa ajili ya maitaji yake, na hiyo ni sehemu ya asili ya uhusiano wake pamoja na Mungu. Ujisikia vizuri sana akimwendea Mungu na kumjulisha juu ya mahitaji yake, mahangaiko yake, na masuala yoyote yanayokuwa yanajiri maishani mwake. Zaidi ya hayo, aliaminishwa na yale aliyosoma katika Biblia kwamba Mungu anataka amtegemee hivyo.

Alionyesha sana maneno haya ya Biblia yasemayo, “Huu ndio ujasiri tulio nao katika kumkaribia Mungu, ya kwamba, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.”1 “Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki. na masikio yake yanasikiliza maombi yao…"2

Nini Mungu Hajibu Maombi ya Kila Mtu?

Huenda ikawa ni kwa sababu hawana uhusiano na Mungu. Huenda wakajua kwamba Mungu yupo, na wanaweza hata kumwabudu Mungu mara kwa mara. Lakini wale ambao maombi yao hayakuwai kujibiwa na Mungu yawezekana hawana uhusiano na yeye. Zaidi hawakuwai kupokea msamaha wa dhambi kutoka kwa Mungu. Je, nini cha kufanya “Hakika mkono wa Bwana si mfupi hata usiweze kuokoa, wala sikio lake si zito hata lisiweze kusikia; bali maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.”3

Ni jambo la kawaida kuhisi kutengwa na Mungu. Watu wanapoanza kumwomba Mungu jambo fulani, ni nini kawaida hufanyika? Wanaanza kwa kusema, “Mungu, nahitaji sana msaada wako katika tatizo hili...” Kisha kunakuwa na ukimya, na kufuatiwa na kuanza upya... “Ninatambua kwamba mimi si mtu mkamilifu, kwamba kwa kweli sina haki kukuomba jambo hili...” Kuna ufahamu wa dhambi ya kibinafsi na makosa. Na mtu huyo anajua kwamba si wao tu; kwamba Mungu pia anajua. Kuna hisia ya, "Ninatania nani?" Kitu ambacho huenda hawajui ni jinsi gani wanaweza kupokea msamaha wa Mungu kwa dhambi zao zote. Huenda wasijue kwamba wanaweza kuingia katika uhusiano na Mungu ili Mungu awasikie. Huu ndio msingi wa Mungu kujibu maombi yako.

Ni kwa vipi Maombi ufanya kazi?

Ni lazima kwanza uanze uhusiano na Mungu. Hii ndio sababu. Fikiria kwamba mvulana anayeitwa Mike anamwomba rais wa Chuo Kikuu cha Princeton amtilie saini kwa ajili ya mkopo wa gari. Ikiwa Mike yeye binafsi hamjui rais wa Princeton, mkopo huo wa gari hautafanikiwa. Hata hivyo, ikiwa binti wa rais huyo angemwomba baba yake amtilie saini katika mkopo wa gari, haingekuwa shida. Kinachoitajika ni mahusiano.

Kwa Mungu, wakati mtu huyo ni mtoto wa Mungu, wakati mtu huyo ni wa Mungu, Mungu anawajua na anasikia maombi yao. Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu na kondoo wangu wananijua... kondoo wangu huisikia sauti yangu. Ninawajua nao wanifuata. Ninawapa uzima wa milele, wala hawatapotea kamwe; hakuna hata mmoja. anaweza kuwanyakua kutoka mkononi mwangu.”4

Unapokuja kwa Mungu basi, Je, unamjua kweli na yeye anakujua? Je, una uhusiano naye unaompa kibali Mungu ajibu maombi yako? Au je, Mungu yuko mbali sana, umekuwa tu kawaida maishani mwako? Ikiwa Mungu yuko mbali, au huna uhakika yakuwa unamjua Mungu, hivi ndivyo unavyoweza kuanza uhusiano naye sasa hivi: Jinsi ya Kumjua Mungu Kibinafsi.

Je, ni hakika kwamba Mungu atajibu Sala yako?

Kwa wale wanaomjua na kumtegemea, Yesu anaonekana kuwa mkarimu sana katika majibu yake: “Ninyi mkikaa ndani yangu na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtapewa.”5 Kwahiyo “wakae” ndani yake na maneno yake yakae ndani yake ina maana yake wanaendesha maisha yao kwakumjua, kumtegemea, nakukisikiliza anachosema. Kisha wanaweza kumuuliza chochote wanachotaka. Hapa kuna sifa nyingine: “Huu ndio ujasiri tulio nao katika kumkaribia Mungu, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia tulichomwomba.”6 Mungu hujibu maombi yetu kulingana na mapenzi yake (na kulingana na hekima yake, upendo wake kwetu, utakatifu wake, n.k.).

Tunapojikwaa kudhani tunajua mapenzi ya Mungu, kwa sababu jambo fulani lina maana kwetu! Tunachukulia kwamba kuna "jibu" moja tu sahihi kwa maombi maalum, tukichukulia hakika HAYO yangekuwa mapenzi ya Mungu. Na hapa ndipo inakuwa ngumu. Tunaishi ndani ya mipaka ya muda na mipaka ya maarifa. Tuna maelezo machache tu kuhusu hali na athari za hatua za baadaye kwenye hali hiyo. Ufahamu wa Mungu hauna kikomo. Jinsi tukio linavyofanyika katika maisha au historia ni kitu anachojua tu. Na anaweza kuwa na makusudi zaidi ya vile tunavyoweza hata kuwazia. Kwa hiyo, Mungu hatafanya jambo fulani kwa sababu tu tunaamua kwamba lazima liwe mapenzi yake.

Ni kwa Muda gani? Mungu Amekusudia Kufanya Nini?

Kurasa na kurasa zinaweza kujazwa kuhusu nia ya Mungu kwetu. Biblia nzima ni maelezo ya aina ya uhusiano ambao Mungu anataka tuwe nao pamoja naye na aina ya maisha anayotaka kutupa. Hapa kuna mifano michache tu:

“...Bwana anatamani kuwafadhili. Anainuka ili kuwaonea huruma. Kwa kuwa Bwana ni Mungu wa haki. Heri wote wamngojeao [wanaomtumaini]!”7 Je, umeelewa? Kama mtu anayeinuka kutoka kwenye kiti chake ili kuja kukusaidia, “Anainuka kukuonyesha huruma.” “Kama ambavyo Mungu, njia yake ni kamilifu...Yeye ni ngao yao wote wanaomkimbilia.”8 “Bwana hupendezwa na wale wanamuogopa [wanaomcha], wanaoweka tumaini lao katika upendo wake usio na kikomo.”9

Hata hivyo, onyesho kuu la Mungu la upendo na kujitolea kwake kwako ni hili: Yesu alisema, “Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake,”10 jambo ambalo Yesu alifanya kwa ajili yetu. Na kwa hiyo, “Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani aliye juu yetu? Kwa kuwa Mungu hakumwachilia hata Mwanawe mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, je! Mungu aliyemtoa Kristo hatatupa sisi vitu vingine vyote?”11

Vipi kuhusu Sala "isiyojibiwa"?

Hakika watu huwa wagonjwa, hata kufa; matatizo ya kifedha ni ya kweli, na uwezekano wa kuja kwa hali ngumu sana ya kila namna. Nini sasa kifanyike?

Mungu anatuambia tumpe mahangaiko yetu. Hata kama hali inaendelea kuwa ya kusikitisha, “Mtwikeni fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.”12 Hali zinaweza kuonekana kuwa haziwezi kudhibitiwa, lakini sivyo. Wakati ulimwengu wote unaonekana kuvunjika, Mungu anaweza kutuweka pamoja. Huu ndio wakati mtu anaweza kushukuru sana kwamba anamjua Mungu. “Bwana yu karibu. Msijisumbue kwa neno lo lote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”13 Mungu anaweza kutoa masuluhisho, masuluhisho ya NJIA yanye shida zaidi ya vile ulivyowazia kuwa inawezekana. Pengine Mkristo yeyote anaweza kuorodhesha mifano kama hii katika maisha yake mwenyewe. Lakini hali zisipoboreka, bado Mungu anaweza kutupa amani yake katikati yake. Yesu alisema, “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.”14

Ni katika hatua hii (wakati hali bado ni ngumu) ambapo Mungu anatuomba tuendelee kumwamini – “kuenenda kwa imani, si kwa kuona” Biblia inasema. Lakini sio imani potofu. Inategemea tabia yenyewe ya Mungu. Gari linalosafiri kwenye Daraja la Golden Gate linaungwa mkono kikamilifu na uadilifu wa daraja. Haijalishi ni nini dereva anaweza kuwa anahisi, au kufikiria, au kujadiliana na mtu aliye kwenye kiti cha abiria. Kinachoifanya gari kuelekea upande wa pili kuwa salama ni uadilifu wa daraja hilo, ambalo dereva alikuwa tayari kuliamini.

Vivyo hivyo, Mungu anatuuliza tuamini uadilifu wake, tabia yake...huruma yake, upendo, hekima, haki kwa niaba yetu. Anasema, “Nimekupenda kwa upendo wa milele, kwa hiyo nimeendelea uaminifu wangu kwako.”15 “Mtumainini yeye siku zote, enyi watu. Imiminieni mioyo yenu mbele zake. Mungu ndiye kimbilio letu.”16

Kwa ufupi

Mungu amejitolea kujibu maombi ya watoto wake (wale ambao wamempokea katika maisha yao na kutafuta kumfuata). Anatuomba tupeleke mahangaiko yoyote kwake katika sala na atayafanyia kazi kulingana na mapenzi yake. Tunapokabiliana na matatizo tunapaswa kumtwika yeye fadhaa zetu na kupokea kutoka kwake amani ambayo inapingana na mazingira. Msingi wa tumaini na imani yetu ni tabia ya Mungu mwenyewe. Kadiri tunavyomjua vizuri zaidi, ndivyo tunavyofaa zaidi kumwamini.

Kwa zaidi kuhusu tabia ya Mungu, tafadhali tazama “Mungu ni nani?” au makala nyingine kwenye tovuti hii. Sababu ya sisi kuomba ni tabia ya Mungu. Maombi ya kwanza ambayo Mungu anajibu ni maombi yako ya kuanza uhusiano na Mungu.

 Jinsi ya kuanza uhusiano na Mungu
 Nina swali…

[na Dkt. Marilyn Adamson]

Maelezo ya Chini:
(1) 1Yohana 5:14 (2) 1Petro 3:12 (3) Isaya 59:1,2 (4) Yohana 10:14,27-28 (5) Yohana15:7 (6) 1 Yohana 5:14,15 (7) Isaya 30:18 (8) Zaburi 18:30 (9) Zaburi 147:11 (10) Yohana15:13 (11) Warumi 8:32 (12) 1 Petro 5:7 (13) Wafilipi 4:5-7 (14) Yohana 14:27 (15) Yeremia 31:3 (RSV) (16) Zaburi 62:8


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More