×
TAFUTA
Mahali Salama pa Kuchunguza Maswali
 jinsi unavyoweza kumjua Mungu
Maisha yangu

Mahusiano na Utafutaji wa Urafiki

Jua jinsi ya kupenda na kupendwa. Pata urafiki wa kweli katika mahusiano yako…

WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More PDF

Sikiliza makala hii:

Dkt. Henry Brandt, katika jarida la Changamoto katika Mahusiano, alisema kwamba kuna ugonjwa (hali) iliyozeelika. Ambapo wachumba uja kwake. Nakusema, “Mwanzoni, mahusiano yetu yalikuwa mazuri. Na nilianza kujisikia vizuri binafsi, na baadae nikaanza kujisikia vizuri nikiwa na mwenzangu. Tulipobishana na kugombana, mwishowe tulivunja mahusiano yetu. Na sasa sisi ni maadui.”

Hii hali hiyo ndo ile ninayoiita asubuhi baada hali. Tunaamka na kukuta hakuna mahusiano ya kweli kabisa. Uhusiano wa kimapenzi hauturidhishi tena, na tunaishia mahala ambapo sio tulipotaka kuishia hapo kwanza. Nyote pamoja mnatakiwa kuwa sehemu moja japo watu utafuta kujiridhisha binafsi. Kupata upendo wa kweli na urafiki hauwezi kupatikana “papo hapo” na utajikuta uko katika hali ya kukosa utulivu, kwa kutafta maelewano.

Urafiki unamaanisha ni zaidi ule wa kimwili.

Kila mmoja wetu ana sehemu tano muhimu katika maisha yetu. Tuna mwonekano (mwili), hisia, hakili, kuhusiana(kijamii) na rohoni. Mambo haya matano yameumbwa ili yafanye kazi pamoja kwa upatano. Katika kutafta urafiki tunataka suluhisho la leo, au la jana. Moja ya matatizo tulionayo ni kwamba tunataka kuridhika “mara moja”. Wakati hitaji la urafiki katika uhusiano halijafikiwa, tunaagalia suluhisho la “papo hapo”. Tunaangalia wapi? mwili, akili, jamii, hisia au rohoni? Ni ya kimwili. Ni rahisi kuwa karibu kimwili na mtu kuliko kuwa wa karibu katika mojawapo ya maeneo mengine manne. Unaweza kuwa na uhusiano wa karibu kimwili na mtu wa jinsia tofauti kwa saa moja, au nusu saa inategemea tu hamu ya mtu iliyopo! Lakini hivi karibuni utagundua kwamba ngono inaweza tu kuwa kitulizo cha muda kwa tamaa ya juu juu. Kuna hitaji la ndani zaidi ambalo bado halijatimizwa.

Unafanya nini msisimko unapokwisha na kadiri unavyofanya ngono zaidi, ndivyo kidogo unavyopunguza kupenda? Tunasawazisha kwa kusema, “Tunapendana. Hapana, ninamaanisha tunapendana sana.” Lakini bado tunajikuta tuna hatia na kutoridhika. Katika vyuo vikuu vyote Amerika ninaona wanaume na wanawake wakitafuta urafiki, wakitoka uhusiano mmoja hadi mwingine wakitumaini kuwa, “Wakati huu utakuwa hivyo. Wakati huu nitapata uhusiano ambao utadumu.”

Ninaamini kuwa tunachotaka sana sio ngono. Tunachotaka sana ni ukaribu.

Leo, neno urafiki limechukua maana ya ngono. Lakini ni zaidi ya hayo. Inajumuisha nyanja zote tofauti za maisha yetu -- ndiyo, ya kimwili, lakini pia nyanja za kijamii, kihisia, kiakili na kiroho pia. Urafiki wa karibu unamaanisha kushiriki maisha yote. Na je, sisi sote hatukuwa na hamu ya mara moja au nyingine ya ukaribu, umoja, kwa kushirikishana kabisa maisha yetu na mtu?

Hofu ya urafiki - hofu ya kupendwa?

Marshall Hodge aliandika kitabu kiitwacho Hofu Yako ya Upendo. Ndani yake anasema, “Tunatamani nyakati za maonyesho ya upendo, ukaribu na huruma, lakini mara kwa mara, katika hatua muhimu, mara nyingi tunarudi nyuma. Tunaogopa ukaribu. Tunaogopa upendo”. Baadaye katika kitabu hicho hicho Hodge anasema, “Kadiri unavyomkaribia mtu, ndivyo uwezekano mkubwa wa maumivu unavyoongezeka.” Ni hofu ya maumivu ambayo mara nyingi hutufukuza kutoka kwa kupata urafiki wa kweli.

Nilikuwa nikitoa mfululizo wa mihadhara katika chuo kikuu kilicho kusini mwa Illinois. Baada ya mkutano mmoja, mwanamke mmoja alikuja kwangu na kusema, “Lazima nizungumze nawe kuhusu matatizo ya mpenzi wangu”. Tuliketi, akaanza kunieleza shida zake. Baada ya muda mchache, alitoa kauli hii: “Sasa ninachukua hatua za kutoumia tena”. Nilimwambia, “Kwa maneno mengine, unachukua hatua za kutopenda tena”. Alidhani sikumwelewa, kwa hivyo aliendelea. “Hapana, sicho ninachosema. Sitaki tu kuumia tena. Sitaki maumivu katika maisha yangu”. Nikasema, “Hiyo ni kweli, hutaki mapenzi maishani mwako.” Unaona, hakuna kitu kama “upendo usio na uchungu”. Kadiri tunavyomkaribia mtu, ndivyo uwezekano mkubwa wa maumivu unavyoongezeka.

Ningekadiria kuwa wewe (na karibu asilimia 100 ya watu) ungesema umeumizwa kwenye uhusiano hapo awali. Swali ni je, unashughulikiaje uchungu huo? Ili kuficha maumivu, wengi wetu huwapa watu kile ninachoita “ishara mbili”. Tunamwambia mtu, “Angalia, nataka unikaribie. Nataka kupenda na kupendwa ... lakini subiri kidogo, niliwahi kuumizwa hapo awali. Hapana, sitaki kuongea juu yake. masomo haya. Sitaki kusikia mambo hayo”. Tunajenga kuta kuzunguka mioyo yetu ili kutulinda dhidi ya mtu yeyote aliye nje asije akaingia ndani akatuumiza. Lakini ukuta uleule unaowazuia watu wasiingie, hutuwekea mwakwamo wa ndani. Matokeo yake? Upweke huingia na urafiki wa kweli na upendo huwa hauwezekani tena.

Upendo ni nini?

Upendo ni zaidi ya hisia, na ni zaidi ya hisia nzuri. Lakini jamii yetu imechukua kile ambacho Mungu amesema kuhusu mapenzi, ngono na ukaribu na kukibadilisha kuwa hisia na hisia tu. Mungu anaelezea upendo kwa kina sana katika Biblia, hasa katika Kitabu cha Wakorintho wa Kwanza, sura ya 13. Hapa Mungu anaeleza kiundani zaidi maana ya upendo, hebu niwasilishe mstari wa nne hadi wa saba (1 Wakorintho 13:4-7). kwako hivi. Kiasi gani ingekidhi mahitaji yako ikiwa mtu anakupenda kama Mungu anavyosema tupendwe:

  • ikiwa mtu huyu alikujibu kwa uvumilivu, ukarimu, na hakuwa na wivu juu yako?
  • ikiwa mtu huyu hakuwa na majivuno au kiburi?
  • vipi ikiwa mtu huyu hakuwa mkorofi kwako au hakujitafuta au kukasirika kwa urahisi?
  • vipi ikiwa mtu huyu hakuweka rekodi ya makosa yako?
  • vipi ikiwa walikataa kuwa wadanganyifu, lakini walikuwa wakweli kwako kila wakati?
  • vipi ikiwa mtu huyu atakulinda, akakuamini, akitumaini mema yako kila wakati, na angevumilia kupitia migogoro na wewe?

Hivi ndivyo Mungu anavyofafanua upendo anaotaka tuwe nao katika mahusiano. Utagundua kuwa aina hii ya upendo inalenga “mtu mwingine”. Ni kutoa, badala ya kujitafutia. Na hapo ndipo penye shida. Ni nani awezaye kuiishi hadi hii?

Kwa urafiki wa kweli, tunahitaji kwanza kuhisi kupendwa.

Ili sisi tupate uzoefu wa upendo wa aina hii katika mahusiano tunahitaji kwanza tupate uzoefu wa upendo wa Mungu kwetu. Huwezi kuonyesha aina hii ya upendo mara kwa mara kwa mtu ikiwa hujawahi kupendwa kwa njia hii. Mungu, anayekujua, anayejua kila kitu kukuhusu, anakupenda kikamilifu.

Mungu anatuambia kupitia nabii wa kale, Yeremia, “Nimekupenda kwa upendo wa milele, nami nimekuvuta kwangu” (Yeremia 31:3). Kwa hiyo upendo wa Mungu kwako hautabadilika kamwe.

Mungu alitupenda sana hivi kwamba aliruhusu Yesu Kristo asulubishwe (namna ya zamani ya kunyongwa) kwa ajili ya dhambi zetu ili tuwe safi. Tunasoma katika Biblia, “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16). Tunapomgeukia Mungu na kukubali msamaha wake, ndipo tunaanza kupata uzoefu wa upendo wake.

Mungu anatuambia, “Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote” (1Yohana 1:9). Sio tu kwamba Mungu anasamehe dhambi zetu, lakini anasahau na kutusafisha.

Ingekuwaje kupendwa hivi?

Mungu anaendelea kutupenda hata iweje. Mara nyingi, uhusiano huisha wakati kitu kinapobadilishwa, kama vile ajali yenye kudhuru au kufilizika kifedha. Lakini upendo wa Mungu hautegemei sura yetu ya kimwili au ni nani au jinsi tulivyo.

Kama unavyoona, maoni ya Mungu kuhusu upendo ni tofauti kabisa na yale ambayo jamii inavyofafanua kuhusu upendo. Je, unaweza kufikiria uhusiano na aina hii ya upendo? Mungu anatuambia ili kupata msamaha wake na upendo wake kwetu ni kwa njia ya kuomba. Ni zawadi yake kwetu. Lakini tukikataa zawadi hiyo, sisi ndio tunajitenga kupata utimizo wa kweli, urafiki wa kweli na kusudi la kweli maishani.

Upendo wa Mungu hutoa jibu. Tunachopaswa kufanya ni kujibu kwa imani na kujitolea. Biblia inasema hivi kuhusu Yesu: “Kwamba wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake” (Yohana 1:12). Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu, afe badala yetu. Lakini hadithi hiyo haiishii hapo. Siku tatu baadaye, Yesu alifufuka kutoka kwa wafu. Kama Mungu, yuko hai leo na anataka kuweka upendo wake moyoni mwako. Mara tu unapomkubali, utastaajabishwa na kile Anachoweza kufanya katika maisha yako na katika mahusiano yako.

Neno la Mungu linatuambia, “Amwaminiye Mwana (Yesu Kristo) yuna uzima wa milele, lakini asiyemtii Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia” (Yohana 3:36). Mungu anachotaka kwetu ni kuwa na uzima, si wa leo tu, bali wa milele. Ikiwa tutachagua kumkataa, basi tumechagua matokeo ya dhambi ambayo ni kifo na kutengwa naye milele.

Ni mapokezi ya Yesu Kristo, kumpokea katika maisha yetu na kumwamini, ambayo huleta maisha yetu katika usawa. Imani katika Mungu inaachilia msamaha wa Mungu. Hakuna kujificha tena, na hakuna tena kwenda kwa njia yetu wenyewe. Yupo pamoja nasi. Tuna amani naye.

Baada ya sisi kuweka imani yetu na utegemezi wetu Kwake, Yeye huchukua makazi ndani ya maisha yetu na tunakuwa na ukaribu Naye. Msamaha wake upo ili kutusafisha kutokana na dhambi ya ndani kabisa, ubinafsi wa ndani kabisa, shida kuu au mapambano ambayo tumewahi kuwa nayo au tutakuwa nayo.

Katika Biblia yote, mtazamo wa Mungu kuhusu ngono uko wazi kabisa. Mungu amehifadhi ngono kwa ndoa na ndoa pekee. Si kwa sababu anataka kutufanya tuwe wanyonge, bali kwa sababu anataka kulinda mioyo yetu. Anataka kutujengea msingi wa usalama, ili tunapofunga ndoa, urafiki wake wa karibu utegemee usalama wa upendo na hekima ya Mungu.

Ukaribu hutokana na hali ya usalama na kupendwa.

Tunapojikabidhi kwa Yesu Kristo, Yeye hutupa upendo mpya na nguvu mpya siku baada ya siku. Hapa ndipo ukaribu tunaoutafuta unaporidhika. Mungu anatupa upendo ambao hautaacha, na hautakoma na miaka ya kukua na mabadiliko ya nyakati. Upendo wake unaweza kuwaleta watu wawili pamoja, naye akiwa katikati ya muungano huo. Katika uhusiano wa kuchumbiana, mnapokua pamoja, si kiroho tu, bali kijamii, kiakili na kihisia, mnaweza kuwa na uhusiano wa uaminifu, unaojali na wa karibu ambao unatimiza na kusisimua! Na wakati uhusiano unapokuja ambao unafikia kilele cha ndoa, muungano wa ngono unaweza tu kuimarisha msingi ambao umeanzishwa.

Katika uhusiano wetu wowote, kujua kwamba tunapendwa na Mungu, hutuweka huru kuwapenda wengine kikweli zaidi. Sisi ni wahitaji kidogo kihisia. Wivu, uchungu, na kutokuwa mwaminifu ambayo ni sifa ya mahusiano mengi sio chaguo letu pekee. Tunaona kwamba hatuna budi kujitoa katika hilo. Badala yake, tunaweza kuweka kando michezo, kuwa wakweli, na hata kusamehe makosa. Kwa ufupi, tunapoona upendo wa Mungu, hutuchochea kuelekea njia tofauti ya uhusiano na wengine.

Je, ungependa kumjua Mungu na kumruhusu akuongoze katika maisha yako na mahusiano yako?

Unaweza kumpokea Kristo sasa hivi kwa imani kupitia maombi. Maombi ni kuzungumza na Mungu. Mungu anaujua moyo wako na hajali sana maneno yako kama vile anavyojali mtazamo wa moyo wako. Ifuatayo ni sala iliyopendekezwa: “Bwana Yesu, ninakuhitaji. Asante kwa kufa msalabani kwa ajili ya dhambi zangu. Ninafungua mlango wa maisha yangu na kukupokea kama Mwokozi na Bwana wangu. Asante kwa kusamehe dhambi zangu na kunipa mimi uzima wa milele. Tawala maisha yangu na unifanye niwe mtu wa aina unayotaka niwe.” Amina.

Je, maombi haya yanaonyesha hamu ya moyo wako? Kama ndivyo, omba maombi haya sasa hivi. Kuweka imani yako katika Kristo kutasababisha kuja kwake katika maisha yako kama alivyoahidi. Hii itaanzisha uhusiano kati yako na yeye, ambao unakuwa zaidi kwa kadri uvyotafta kumjua zaidi. Ukiwa naye katika utukufu wake, maisha yako yanachukua mwelekeo mpya kabisa wa kiroho na kuleta maelewano zaidi na utimilifu kwa uhusiano wako wote.

Kujua na kupitia upendo wa Mungu kwako, utaweza kuwapenda wengine kwa upendo wa Mungu, ambao unaongoza kwa kiwango cha ndani zaidi cha urafiki wa kweli.

 Nilimpokea Yesu maishani mwangu (ujumbe muhimu unafuata)…
 Ninaweza kutaka kumuuliza Yesu maishani mwangu, tafadhali eleza hili kikamilifu zaidi…
 Nina swali…

[na Dkt. Richard Purnell]

© Dkt. Richard Purnell – Dkt. Richard Purnell ameongea na wanafunzi wa vyuo vikuu na vya kati zaidi ya 450. Ni muandishi wa vitabu 12, kujumuisha kitabu chake kinachoitwa Becoming a Friend and Lover and Free to Love Again: Coming to Terms with Sexual Regret.


SHIRIKISHA WENGINE
WhatsApp Share Facebook Share Twitter Share Share by Email More